Jiunge Na Familia Ya 1% Sasa. - Kweligraphy

Jan 19, 2019 · 4m 2s
Jiunge Na Familia Ya 1% Sasa. - Kweligraphy
Description

Maisha yapo tough sana kipindi nina umri mdogo wa kusoma shule ya msingi. Yapo tough pia hadi sasa lakini, nimeongezeka nguvu zaidi kuliko mwanzo na kukua kifikra na uzoefu. Nimejifunza...

show more
Maisha yapo tough sana kipindi nina umri mdogo wa kusoma shule ya msingi. Yapo tough pia hadi sasa lakini, nimeongezeka nguvu zaidi kuliko mwanzo na kukua kifikra na uzoefu. Nimejifunza niliyojifunza kuhusu mimi . Nakumbuka nilipokuwa shule ya chekechea hadi primary na kuendelea. Stori ndefu kuifanya iwe fupi nilikuwa kilaza sana chekechea kuliko wenzangu, nilikuwa kati ya wale vichwa vizito vya darasa, hali iliyonifanya kusoma kwa miaka mitatu chekechea. Kipindi nipo primary nilitamani sana nami niwe mmoja wa wale "cool kids" au "brighter ones" au tulikuwa tunaita "john visomo" sijui kama hilo jina bado linatumika hadi sasa. Tatizo langu kubwa lilikuwa kujua hesabu au kufanya vizuri kwenye mitihani ya hisabati. Nilitamani nami nionekane, nitambulike kila nipitapo eneo la shule kama ilivyo kwa wale wafanyao vizuri shuleni wanavyopendwa na walimu pamoja na wanafunzi wengine, kwa hiyo sababu kuu ya mimi kubadilika na kuwa mmoja wa "cool kids" shuleni ni tamaa ya kutambulika. Nilifahamu wazi kabisa kuwa kilaza si jambo ambalo watu wanalipenda ama watu watakupenda na kukutambua kwa ukilaza wako. Kilichofuata ni hadithi tu. Nilikuwa moja kati ya wanaofanya vizuri shuleni. I was famous indeed, lakini ilifanyika kazi ya ziada.! Vivyohivyo kwenye maisha nje ya shule, ili utambulike, uzawadiwe zawadi ya utambulisho ni lazima upige kazi pasipo ukawaida ili ukaribishwe kwenye chama cha asilimia tano (5%) au asilimia moja (1%) kwa maana wanaotambulika na jamii ni wale wanaojitoa kwa mchango wao wa hali ya juu kufanikisha mambo yao. Unapofanikisha jambo lako kwa kiwango cha juu ni sawa na kuitambulisha familia yako au kaya ama nchi yako kwa ujumla Jina lako litavuka mipaka pale jitihada zako zinapozaa matunda. Nakumbuka vizuri kipindi cha shule nilitoa muda wa masaa 10 hadi 15 kwa kusoma kwa siku, ajabu ya sasa kipindi baada ya shule kumaliza, muda wa kufanya kazi ambayo kwako ni ya umuhimu unaifanya kwa masaa 8 kwa siku, huu ni uozo wenye hadhi ya nyota 5. Badilisha mwenendo wako wa maisha, inawezekana ulikuwa superstar shule, umekuwa kilaza uraiani; nakushauri utumie strategy zilezile za shuleni vile ulivyokuwa unafanya. Geuza tu kidogo, kule ilikuwa ni kusoma, huku ni kupiga kazi. Zidisha masaa ya kazi. Tukutane kwenye familia ya 1% ya watu wanaotambulika mshkaji wangu. New Years Resolution. #kweligraphy
show less
Information
Author Said Kweli
Organization Said Kweli
Website -
Tags

Looks like you don't have any active episode

Browse Spreaker Catalogue to discover great new content

Current

Podcast Cover

Looks like you don't have any episodes in your queue

Browse Spreaker Catalogue to discover great new content

Next Up

Episode Cover Episode Cover

It's so quiet here...

Time to discover new episodes!

Discover
Your Library
Search